Natumaini kwamba muwazima na mko tayari kuendelea kusoma makala haya ambayo naamini kwa namna moja ama nyingine yanakupa elimu ambayo huenda ulikuwa huijui.
Bado nazungumzia faida za kutoka nje ya ndoa kama ambavyo nimefanya kwa wiki ya tatu sasa. Hata hivyo, faida hizo zinaelezwa kuwa za hasara kutokana na ukweli kwamba, kuna hasara inayoweza kuwapata watu walio katika ndoa endapo watageuza kutoka nje ya ndoa zao kuwa utaratibu wa maisha yao ya kila siku.
Kama utakumbuka nilieleza kwamba, kwanza kutoka nje ya ndoa kunaweza kuwafanya wanandoa wakadumu kwa muda mrefu tofauti na wale ambao uaminifu kwao ni asilimia mia moja. Pia nikasema, tabia hiyo inachangia kuongezeka kwa mapenzi ndani ya ndoa.
Kwa waliobahatika kusoma matoleo yaliyopita watakuwa wameelewa ni kwa jinsi gani tabia hiyo isiyokubalika katika jamii inachangia katika mambo hayo mawili. Hata hivyo, nimekuwa nikisisitiza kwa nguvu zangu zote kuwa, makala haya yasije yakachukuliwa kama kishawishi cha wanandoa kusalitiana, lahasha.
Narudiana tena, lahasha! Hii ni katika kujifunza tu kisha mwishowe lazima uaminifu uchukue mkondo wake ili watu waishi kwa amani na upendo. Tuiangalie sasa faida tatu…
Kunabadili wanandoa
Robert Johnnson, mtaalamu wa masuala ya mapenzi nchini Marekani aliwahi kueleza kuwa, asilimia kubwa ya wanaowasaliti wenza wao kuna kitu ambacho wanakikosa ndani ya ndoa zao.
Ni kweli kuna ambao wanasaliti kutokana na tamaa zao za kijinga lakini wengine kuna kitu wanakifuata. Ni ukweli usiofichika kwamba, mke anaposhindwa kumtimizia mume wake mambo flani flani hasa ya faragha, upo uwezekano mkubwa wa mwanaume huyo kuchepuka.
Hivyo hivyo kwa mwanaume ambaye anamgeuza mkewe kama pambo linalostahili kulishwa, kuvalishwa na kulazwa sehemu nzuri tu. Mwanaume anayemchukulia mkewe kuwa ni wa aina hiyo, lazima atasalitiwa kama hatabadilika.
Johnson aliandika kuwa, mwaka 1989 mwanamke mmoja alikuwa akihisi mumewe ana uhusiano na mwanamke mwingine nje ya ndoa yao. Wakati mwanamke huyo akifanya uchunguzi kubaini kama hisia zake zina ukweli, alianza kujifanyia tathmini kubaini kama yeye anaweza kuwa sababu ya mumewe kumsaliti.
Inaelezwa kuwa, mwanamke yule alianza kuhakikisha suala la usafi wa mwili wake, kuhakikisha kila anapokutana na mumewe faragha anampa mapenzi ya kutosha, kuongeza mahaba na kuhakikisha anamfanya mumewe anakuwa na furaha wakati wote.
Mabadiliko kwa mwanamke huyo yalitokana na hisia kwamba mumewe anamsaliti, hisia ambazo huenda zilikuwa na ukweli na huenda kweli kasoro zake za kujitakia ndizo zilizosababisha mumewe amsaliti.
Hata hivyo, mabadiliko kwa mwanamke huyo yalimfanya arudishe imani kwamba, mumewe hawezi kumsaliti kwa kuwa aliamini kila alichokitaka alimpatia.
Nini tunajifunza katika hili? Walio katika ndoa wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo. Ikitokea siku umemfumania mwenza wako, najua inauma sana lakini si vibaya ukajiangalia kwa jicho la tatu kwani inawezekana kabisa wewe ndiye chanzo cha usaliti huo.
Jiangalie na ikiwezekana badilika kama walivyobadilika wengine baada ya kubaini wanasalitiwa kutokana na udhaifu wao.
Niishie hapo kwa leo, wiki ijayo tutaangalia faida ya nne na ya tano kabla ya kuingia katika mada nyingine mpya.

No comments:
Post a Comment