ILIPOISHIA KATIKA SEHEMU YA TATU:
Baada ya JENIFER kugundulika kuwa alikua anatumia
uongo kumdanganya baba yake kuwa mwalimu KABAVAKO alimtongoza hivyo
wakachukuliwa JENIFER pamoja na wale rafiki zake watatu ambao
walikamatwa usiku CLUB na mwalimu KABAVAKO wakaenda kupewa adhabu ya
kuchapwa fimbo huku nyuma katika ofisi ya mwalimu mkuu akabakia mwalimu
mkuu na baba yake na JENIFER wakiongea.
INAENDELEA HAPA:
Mwalimu KABAVAKO aliwachapa kila mmoja fimbo nne
nne, kisha akawarudisha ofisini kwa mwalimu mkuu walipofika ofisini kwa
mwalimu mkuu, mwalimu mkuu aliwaambia inabidi awape adhabu ya kukaa
nyumbani mpaka uongozi wa shule utakapo kaa kikao na kuwafikiria na
kujadili kosa lao ndio wafanye maamuzi ya kuwasamehe au kutowasamehe.
Mr. Brown baba yake na JENIFER alijitahidi sana kumbembeleza mwalimu
mkuu awasamehe ili waendelee na masomo lakini mwalimu mkuu alikataa katu
katu na akamwambia Mr. Brown kuwa "MZEE KOSA WALILOFANYA HAWA WATOTO NI
KUBWA SANA TENA AFADHALI YA HAWA WENGINE KULIKO HUYU BINTI YAKO
JENIFER, JENIFER KWANZA HANA HESHIMA KADIRIKI KUMSINGIZIA MWALIMU WANGU
KUWA KAMTONGOZA WAKATI SIO KWELI HUONI KAMA HUYU MTOTO ANAWEZA KUJA
KUTUCHAFULIA SIFA YA SHULE YETU? NI BORA NIWASAMEHE HAWA WOTE LAKINI KWA
BINTI YAKO JENIFER SIWEZI KUMSAMEHE" ghafla mwalimu mkuu akabadilisha
mawazo pale pale akawaambia wale rafiki zake na JENIFER "NYIE
NIMEWASAMEHE NENDENI NYUMBANI MKAVAE NGUO ZA SHULE NA MJE DARASANI
MUENDELEE NA MASOMO ILA JENIFER SINTOWEZA KUMSAMEHE SAWA?!" wale
wanafunzi watatu ambao ni rafiki zake JENIFER walifurah na hawakuamini
kama wamesamehewa wakamshukuru sana mwalimu mkuu na wakamuahidi kuwa
hawatorudia tena, wakaondoka ofisini na kuelekea majumbani kwao kuvaa
nguo za shule. Huku ofisini mwalimu mkuu akanyanyua simu yake ya mezani
akampigia Secretary wake na kumuamuru achapishe barua ya kumsimamisha
shule mwanafunzi wake JENIFER. Mr. Brown alijitahidi sana kumbembeleza
mwalimu mkuu amsamehe binti yake mpaka machozi yakawa yanamtoka Mwalimu
mkuu akamwambia Mr. Brown "MZEE HILI NATOA FUNDISHO ILI BINTI YAKO
AJIFUNZE SIWEZI KUMSAMEHE MTOTO MSHENZI SANA HUYU" Mr. Brown
alimbembeleza sana mwalimu mkuu lakini mwalimu mkuu alimkatalia katu
katu kumsamehe JENIFER na akawaomba Mr. Brown na Binti yake JENIFER
watoke nje ya Ofisi wasubirie barua ya kusimamishwa shule binti yao.
Baada ya muda Secretary alimaliza kuchapa barua na kuipeleka ofisini kwa
mwalimu mkuu, mwalimu mkuu akamwita kiranja mkuu wa shule akamwambia
aende kupiga kengere ya dharura ili wanafunzi wote wakusanyike mstarini
aitoe barua ile hadharani mbele za wanafunzi. Kengere ilipigwa wanafunzi
wote wakatoka madarasani na kuelekea mstarini wakakusanyika wanafunzi
wote na walimu wote wa shule hiyo, mwalimu mkuu akaanza kuelezea yote
yaliyojiri kwa JENIFER na kuwajulisha wanafunzi kuwa kasimamishwa shule
baada ya hapo wakateuliwa walimu watatu wamchape fimbo JENIFER kila
mwalimu amchape fimbo tatu, kisha wanafunzi wakaruhusiwa waende
madarasani kuendelea na masomo yao. Mr. Brown alijisikia aibu sana kwani
binti yake JENIFER alichofanya ni kitu cha ajabu hivyo alikua na hasira
sana kilichomuumiza ni Ada aliyoitoa shuleni hapo ya kumlipia binti
yake akifikiria jinsi alivyoipata pesa katika mazingira magumu ilimradi
binti yake asome lakini JENIFER yote hakujali, sasa kivumbi kikaanza kwa
Mr. Brown na Mwalimu mkuu, Mr. Brown akaanza kudai pesa ya ada ya mwaka
aliyolipa shule akataka arudishiwe pesa yake ukaanza mzozo ofisini kati
ya Mwalimu mkuu na Mr. Brown hatimae wakaanza kushikana mashati
ofisini, Mr. Brown anataka pesa mwalimu mkuu anasema hatoi pesa ikawa
vurumai ofisini
Je, unadhani nini kitaendelea? Mwalimu mkuu atakubali
kurudisha pesa za ada alizotoa Mr. Brown au Mr. Brown ataamua kusamehe?
Usikose kufuatilia
No comments:
Post a Comment