SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI:
Katika sehemu ya pili tuliona jinsi JENIFER
alivyojaribu kutunga uongo kwa wazazi wake kwa dhumuni la kutaka
kujilinda yeye binafsi kutokana na kosa alilolifanya hivyo akaamua
kumzushia uongo mwalimu wake wa shule ili kumaliza kesi kwa wazazi wake
na mzazi wa JENIFER "Mr. Brown" akamwambia binti yake kuwa siku ya
Ijumaa tatu itabidi waongozane wote mpaka shuleni ili wakaonane na
mwalimu.
INAENDELEA HAPA:
Ilipofika kesho yake asubuhi siku ya Ijumaa tatu
JENIFER na baba yake Mr. Brown walifunga safari mpaka shule, walipofika
shuleni hapo moja kwa moja wakaenda mpaka ofisi ya mwalimu mkuu wa shule
hiyo (HEAD MASTER) walipofika ofisini kwa mwalimu mkuu wakamuomba
JENIFER atoke nje na aelekee mstarini baada ya hapo aende darasani
kusoma. JENIFER akatoka nje na kuelekea mstarini huku ofisini akabakia
mwalimu mkuu na Mr. Brown wakizungumza. Mr. Brown alimuelezea kwa kirefu
mwalimu mkuu kuwa kuna mwalimu wake hapo shuleni anaitwa MWL. KABAVAKO
anamtaka binti yake kama alivyoelezwa na binti yake JENIFER, baada ya
mwalimu mkuu kuambiwa vile alichokifanya akamtafuta kiranja wa shule
akamtuma aende kumuita JENIFER pamoja na huyo Mwalimu KABAVAKO wafike
ofisini hapo kwa mwalimu mkuu. Yule kijana ambae ni kiranja akaenda
kuwaita JENIFER na Mwalimu KABAVAKO walipofika ofisini mwalimu mkuu
akamuomba JENIFER aelezee ilivyokua kuhusu mwalimu KABAVAKO. JENIFER
akaanza kuelezea kama alivyowaelezea wazazi wake kuwa mwalimu KABAVAKO
anamtaka kimapenzi lakini yeye hamtaki na amekua anamtesa sana shuleni
hapo, na amemuahidi kuwa atafanya kila njia ili amfukuzishe shule pia
kuna wanafunzi aliwakamata disco usiku mwalimu KABAVAKO akamuahidi
Jenifer kuwa atamuingiza nayeye katika hilo kosa la hao wanafunzi ili
wafukuzwe wote shule. Ndivyo JENIFER alivyojitetea kwa kusema haya mbele
ya baba yake Mr. Brown, mwalimu mkuu na mwalimu KABAVAKO. Mwalimu
kabavako alipigwa na butwaa akabakia anashangaa kutokana na maneno
aliyosingiziwa lakini alikua ni mwenye busara na subira akamuacha
JENIFER azungumze mpaka alipomaliza ikafika zamu yake mwalimu KABAVAKO
ajielezee alichokifanya mwalimu kabavako akamuuliza swali JENIFER
"JENIFER WEWE HAPA SHULENI UNA MARAFIKI?" Jenifer akamjibu "NDIO NINAO"
mwalimu KABAVAKO akamwambia "UNAWEZA KUNITAJIA MARAFIKI ZAKO WATATU
MUHIMU AMBAO NI WAKARIBU SANA?!" Jenifer akaanza kuwataja marafiki zake
watatu ambao ndio yupo nao karibu sana na katika hao marafiki watatu
aliowataja JENIFER ndio wale ambao mwalimu KABAVAKO aliwakamata wako
wote na JENIFER usiku, baada ya hapo mwalimu KABAVAKO akamuuliza baba
yake na JENIFER "MZEE SIKU YA IJUMAA MOSI BINTI YAKO JENIFER ALILALA
NYUMBANI?!" Baba yake na JENIFER akajibu "MWALIMU MBONA SIKUELEWI
TUNAULIZANA MASWALI KAMA TUPO KITUO CHA POLISI?" mwalimu KABAVAKO
akamjibu "MZEE PUNGUZA JAZBA MIMI NINAKUULIZA HIVI NINA MAANA YANGU"
baba yake na Jenifer ikabidi amjibu mwalimu "KILA SIKU YA IJUMAA MOSI
MWANANGU HUWA ANATOKA ANAENDA KUJISOMEA NA WENZAKE USIKU KUCHA ASUBUHI
ANARUDI NYUMBANI" baada ya mwalimu KABAVAKO Kumuuliza maswali JENIFER na
baba yake kisha akatoka nje na kumtafuta mwanafunzi kisha akamuagiza
yule mwanafunzi aende ofisi kuwaita wale wanafunzi watatu aliowakamata
wakiwa Club usiku pamoja na JENIFER, yule mwanafunzi akaenda kuwaita
wale rafiki zake na JENIFER walikuwa wamevaa mavazi yao ya nyumbani
waliyokamatwa nayo wakaelekea mpaka ofisi ya mwalimu mkuu. Walipofika
ofisini mwalimu KABAVAKO akawauliza "NYIE WANAFUNZI MNAMJUA HUYU
MWANAFUNZI MWENZENU?" wakajibu "NDIO MWALIMU TUNAMJUA ANAITWA JENIFER"
akawauliza tena "KWANINI NYIE MMEKUJA SHULENI MKIWA MMEVAA HIZO NGUO ZA
NYUMBANI TENA FUPI?" wale wanafunzi wakajibu "MWALIMU WEWE SI
ULITUKAMATA SIKU YA IJUMAA MOSI USIKU CLUB UKATUAMBIA TUJE LEO OFISINI
KWAKO NA HIZI NGUO PAMOJA NA WAZAZI WETU?" mwalimu KABAVAKO akawauliza
tena "NILIPO WAKAMATA HIYO SIKU YA IJUMAA MOSI MLIKUA NYIE NYIE WATATU
PEKE YENU AU?" wakajibu "HAPANA MWALIMU TULIKUA PAMOJA NA JENIFER" pale
pale JENIFER nguvu zikamuishia akajua tayari kishakamatwa hana jinsi
akaanza kulia ofisini kwa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu akamwambia JENIFER
"JENIFER TAFADHALI USINIFICHE NIELEZE UKWELI UKINIDANGANYA NAWEZA
KUKUCHAPA HAPA MBELE YA BABA YAKO NA NITAKUFUKUZA SHULENI KWANGU,
NIELEZE UKWELI SI UNAONA WENZAKO WAMENIELEZA UKWELI? HAYA NAWEWE NIELEZE
UKWELI WAKO, MWALIMU KABAVAKO ALIKUKAMATA CLUB KWELI?" JENIFER
akajikuta anasema ukweli "NDIO MWALIMU ALINIKAMATA JUZI IJUMAA MOSI
USIKU NIKO NA HAWA MARAFIKI ZANGU CLUB" mwalimu mkuu akamuuliza tena "NA
JE, NIKWELI MWALIMU KABAVAKO AMEISHAWAHI KUKUTONGOZA?" JENIFER akakosa
jibu akakaa kimya, ghafla JENIFER akasema "BABA NAKUOMBA UNISAMEHE
NILIKUDANGANYA MWALIMU HAJAWAH KUNITONGOZA ILA NILITAKA NIJITETEE UKWELI
NIKWAMBA ALITUKAMATA CLUB USIKU" pale pale Mr. Brown nguvu zilimuishia
akamwambia mwalimu KABAVAKO "MWALIMU NISAMEHE MIMI KWA YOTE HAYA, KUMBE
HUYU MTOTO NI MUONGO SINA LA KUSEMA NAOMBA MUMPE ADHABU YOYOTE ILE NIKO
TAYARI, MSHENZI SANA HUYU MTOTO" mwalimu mkuu akamwambia mwalimu
KABAVAKO atoke nje na wale wanafunzi watatu pamoja na JENIFER akawachape
fimbo kisha arudi nao ofisini kwake. Mr. Brown akabakia na mwalimu mkuu
wanaongea!
INAENDELEA
No comments:
Post a Comment