JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI ni Hadithi inayomuhusu
binti wa kitanzania alietunukiwa uzuri wa asili na mvuto wa kipekee
aliojaaliwa na mungu ama hakika uzuri aliokuwa nao ulikuwa ni kishawishi
tosha kwa mwanaume yoyote aliemtazama binti huyu na kutamani kuwa nae
kutokana na mvuto aliokuwa nao binti huyu anaitwa Jenifer na amezaliwa
katika familia duni ya Mr. Brown na Mrs. Brown yenye watoto watatu (3).
Ambao ni Peter, Joseph na Jenifer na katika watoto hawa watatu mwanamke
alikua ni Jenifer peke yake na ndie alikua mtoto wa kwanza kuzaliwa
katika familia hii yenye watoto watatu ambapo Peter na Joseph walikua ni
wadogo zake na Jenifer na walikuwa bado ni wadogo sana. Na wazazi wa
Jenifer Mr. Brown na Mrs. Brown walitokea kumpenda sana binti yao
Jenifer kwani ndio mtoto pekee wa kike hivyo walionesha upendo mwingi
kwa binti yao kwa kumtimizia mahitaj yote muhimu na kumpa kila
alichokitaka binti yao ili wamridhishe na kuhakikisha wanampa malezi
bora na kujenga upendo imara kwa binti yao. Kutokana na hali ya ngumu
ya maisha iliyokuwepo katika familia hiyo ya Mr. Brown na Mrs. Brown,
wazazi hawa walikaa na kujadili njia sahihi ya kuweza kukabiliana na
umasikini walio nao na kuweza kujikwamua kimaisha wakapata wazo la
kumpeleka shule binti yao Jenifer ili hapo baadae aje kuwasaidia wazazi
wake kupitia elimu atakayoipata shule hivyo wazazi wakakubaliana na
kuanza mipango ya kumuandikisha shule binti yao ili aanze kusoma, wazazi
wa Jenifer walijitahidi kutafuta pesa kwa hali na mali ikapelekea
wazazi wa Jenifer kujiunga na kampuni zinazotoa mikopo ya fedha lengo
kupata pesa waweze kumtimizia mahitaji binti yao aweze kuanza shule.
Mungu alileta kheri kwa wazazi hao na kufanikisha kuipata pesa ya
kumpatia binti yao kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya shule na binti
yao akafanikiwa kuanza elimu ya msingi akasoma darasa la kwanza mpaka
darasa la saba lakini alipo maliza darasa la saba matokeo yake hayakua
mazuri hivyo hakuweza kuchaguliwa katika shule za serekali kwa ajili ya
kuendelea na elimu ya sekondari lakini wazazi wa Jenifer hawakukata
tamaa na waliendelea kuwa na moyo wa kumsaidia binti yao Jenifer kwa
vyovyote vile mpaka waone mwisho wake kwani malengo yao binti yao asome
mpaka daraja la juu afike mpaka chuo kikuu, baada ya Jenifer kumaliza
elimu ya msingi na hakufanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yake
ikabidi wazazi wajipange upya kutafuta ada ya kumlipia binti yao ili
aweze kujiunga na elimu ya sekondari kwa dhumuni la kuhakikisha binti
yao Jenifer anaendelea na elimu. Mungu hakuitupa familia hii ya Mr na
Mrs. Brown aliwajaalia wakafanikiwa kuipata pesa ya kumlipia ada binti
yao na wakamuandikisha katika shule ya kulipia ya sekondari
iliyofahamika kwa jina la
"GARDEN SECONDARY SCHOOL" Jenifer alijiunga na shule
hii na kuanza elimu yake ya sekondari lakini kama ilivyo kwa vijana
wengi wa kisasa kutofahamu umuhimu wa elimu na kushindwa kujua nini
wanapaswa kukifanya pindi wanapo kuwa shule ndivyo ilivyokuwa kwa
Jenifer. Jenifer hakujua umuhimu wa elimu na hakuona juhudi za wazazi
wake kwake za kutafuta pesa kwa ajili ya kumlipia ada ili aje kuwasaidia
baadae na kuwasaidia wadogo zake Peter na Joseph. Kipindi Jenifer
alipokua shuleni hapo akiendelea na elimu ya sekondari tabia yake
ilibadilika akawa anautumia muda wake mwingi wa shule kujichanganya na
marafiki ambao hawakuwa na msaada mzuri kwake na wakati mwingine alikua
akiaga kwao anakwenda shule lakini alikua hafiki shule alikua anakwenda
kwa marafiki anashinda na kurudi nyumbani wazazi wake hawakujua
kinachoendelea kwa binti yao. Wakati mwingine Jenifer alikuwa ni mtu wa
kupenda sana kwenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe wakati alikua
anatoka nyumbani kwao usiku akiwaaga wazazi wake kuwa anakwenda kwa
marafiki zake anaosoma nao wanakwenda kukesha wakisoma na kujadiliana
yale waliyofundishwa shuleni, wazazi wa Jenifer hawakuwa na kipingamizi
kwa binti yao walikua ridhwaa kukubaliana na kila anachohitaji binti yao
ili mradi kumridhisha na kumfanya awe huru ili mwisho wa siku aweze
kutimiza ndoto za wazazi wake hivyo wazazi walikua wakimpa ruhusa binti
yao atoke usiku wakidhani anaenda kusoma na wenzake kumbe Jenifer alikua
anatumia muda huo kutoka na kwenda CLUB (kumbi za starehe) na marafiki
zake wanaenda kujirusha
na alikua anarudi nyumbani kwao kesho yake asubuhi,
na ilikua kila ikifika siku ya Ijumaa mosi ndio anatoka usiku na
wenzake, siku moja kama kawaida yake Jenifer na wenzake wametoka na
kwenda kwenye kumbi za starehe huku nyumbani wazazi wanajua watoto wao
wameenda katika masomo yao kama ilivyozoeleka, kipindi wapo CLUB kuna
mwalimu wao wa shule alikuwepo katika ukumbi huo wa starehe na akakutana
na kundi hili la wakina dada kama wanne akiwemo na Jenifer wakiwa
wamevaa mavazi mafupi ya ajabu kama machangudoa wanaojiuza, yule mwalimu
wao alichokifanya akawaita kisha akawaambia "NAOMBA SIKU YA JUMATATU
MKIFIKA SHULE CHA KWANZA NAOMBA NIWAKUTE OFISINI KWANGU KAMA MLIVYO
WANNE TENA MJE MKIWA MMEVAA HIZI NGUO MLIZO ZIVAA NA KILA MMOJA WENU AJE
NA MZAZI WAKE" kisha mwalimu akawaambia wawe huru waendelee na mambo
yao ila ikifika siku ya jumatatu siku ya shule wafanye kama alivyo
agiza mwalimu huyo pale pale Jenifer na wenzake wakakosa amani na mudi
ya kuendelea kufurahi usiku ule ikatoweka na kila mmoja wao akawa
anawaza itakuaje hiyo siku ya Ijumaa tatu na wataanzia wapi kuwaeleza
wazazi wao juu ya kosa hili walilofanya mpaka wamekutana na mwalimu
kawaomba waende shule na wazazi wao.....?!
Mpenzi msomaji wa hadithi hii Unadhani nini kitaendelea kwa Jenifer na wenzake baada ya kukamatwa na mwalimu sehemu ambayo si nzuri hususan kwa upande wao ikiwa bado ni wanafunzi na istoshe wameaga kwa wazazi wao wanaenda kusoma usiku ule?! Je, itakuaje nini watakifanya siku hiyo ya jumatatu? Usikose muendelezo wa hadithi hii SEHEMU YA PILI siku ya jumatano.
ITAENDELEA USIKOSE
No comments:
Post a Comment