INAENDELEA HAPA:
Baada ya JENIFER na wenzake kukamatwa na mwalimu na
kupewa adhabu hiyo ya kwenda na wazazi wao shuleni siku ya Ijumaa tatu
na kupelekea kupoteza mudi ya kuendelea kufurah usiku huo ikawabidi
waondoke kabisa sehemu hiyo ya CLUB usiku huo huo na kwenda kulala
kwenye chumba cha rafiki yao CHRISTINA waliekuwa nae katika kundi lao
usiku huo, ilipofika kesho yake siku ya ijumaa pili asubuhi kila mtu
alirejea nyumbani kwao huku wakiwa na sura za hudhuni na mawazo kibao
kichwani wakijiuliza itakuaje kesho yake ambayo ni siku ya Ijumaa tatu
wanatakiwa waende shule na wazazi wao?!. Jenifer alipofika kwao moja kwa
moja alielekea chumbani kwake na kujilaza kitandani huku akiwa na
mawazo kibao hata chakula hakuweza kula siku hiyo muda wote alikua
kajifungia chumbani analia. Ghafla akasikia mlango wa chumbani kwake
unafunguliwa aliposhtuka akamuona mama yake Mrs. Brown. Mrs. Brown
alimsogelea binti yake Jenifer kuanza kuzungumza nae kama ifuatavyo:-
MRS. BROWN:
"Jenifer binti yangu mbona unaonekana leo hauko sawa, nini tatizo mwanangu?! Na mbona unalia?
JENIFER:
"Hapana mama, wala usijali hamna kitu chochote naomba uwe na amani mama yangu, niko sawa tu!"
MRS. BROWN:
"Jenifer mwanangu lazima kutakuwa kuna kitu ila
unaficha. Mwanangu nakuomba unieleze usinifiche niambie tu mwanangu wala
usiogope"
JENIFER:
"Mama wala usijali hakuna kitu chochote kile"
MRS. BROWN:
"Sidhani binti yangu kama kweli hakuna tatizo sasa mbona unalia, Au umepata ujauzito?!
JENIFER:
"Mama bora ningekua nina ujauzito ila kwa hiki
kilichonipata mama yangu najuta tena najuta hata sijui kwanini
mlinipeleka shule mama yangu"
MRS. BROWN:
"Mwanangu mbona unasema hivyo kwani kuna tatizo limetokea shule?!
JENIFER:
"Ndio mama, kuna mwalimu shuleni alinitongoza
nikamkatalia sasa kila siku huwa ananichapa fimbo bila makosa na
ananitesa sana shule na kaniahidi kuwa atanitafutia kosa lolote la uongo
ili nifukuzwe shule anikomoe na juzi siku ya Ijumaa kuna wanafunzi
kawakamata usiku CLUB akawaambia kuwa atawafukuza shule sasa kaniambia
namimi ataniingiza katika hilo kosa la hao wanafunzi kesho shuleni ili
nifukuzwe namimi"
MRS. BROWN:
"Haiwezekani mwanangu wewe nyamaza acha kulia
tumsubiri baba yako aje nimuelezee ikiwezekana kesho akupeleke shule
akamkomeshe huyo mwalimu, wala usiwaze sana mwanangu Jenifer looooo,
huyo mwalimu hana hata aibu"
Baada ya Jenifer kutumia uongo wa kumdanganya mama
yake Mrs. Brown kwa dhumuni la kujitetea kutokana na kosa alilolifanya
usiku wa jana yake walipokutwa na mwalimu wao wa shule CLUB ikamlazimu
kumpa kesi ya uongo yule mwalimu kwa wazazi wake ili wasimuone yeye
anamakosa. Mama yake na Jenifer Mrs. Brown alihamaki na kuingiwa na
hasira akawa anamsubiria mume wake arudi ili amuelezee kilichotokea.
Ghafla baba yake na Jenifer Mr. Brown akaingia nyumbani kwake na kumkuta
mke wake Mrs. Brown akiwa na binti yao Jenifer, Jenifer alipomuona baba
yake Mr. Brown akaanza kuangua kilio huku akisema "BABA NAJUTA MIMI
MWANAOO, NAJUTA BABA HIVI KWANINI ULINIPELEKA NIKASOME ILE SHULE BABA
YANGUUUUUU" Jenifer alikua analia huku akitoa sauti kubwa ya
kumlalamikia baba yake. Mr. Brown alipigwa na butwaa hakujua nini
kinachoendelea ikabidi akae chini na kumuuliza mke wake "MKE WANGU NINI
KIMEMPATA BINTI YETU JENIFER?" Mrs. Brown akamjibu mume wake "MUME WANGU
NENDA KWANZA KAKOGE KISHA ULE HALAFU NDIO NIKUELEZEE KILICHOTOKEA" Mr.
Brown nae akamjibu "HAPANA MKE WANGU NIELEZEE KWANZA NIJUE TATIZO
NINI?". Mrs. Brown ikabidi aanze kumuhadithia kama alivyohadithiwa na
binti yao Jenifer kuwa kuna mwalimu wa shule alimtongoza binti yao
akamkataa sasa huyo mwalimu anamtesa sana Jenifer shuleni na kamuahidi
atamfanyia njama yoyote ili binti yao afukuzwe shuleni. Pale pale Mr.
Brown nayeye akapandwa na hasira akamnyamazisha binti yake Jenifer na
kumwambia "JENIFER BINTI YANGU NYAMAZA, KESHO IJUMAA TATU ASUBUHI
TUTAKWENDA WOTE MPAKA SHULENI KWENU UKANIONESHE HUYO MWALIMU.
ATANITAMBUA" baada ya hapo wakatawanyika Jenifer akaingia chumbani
akaanza kushangilia peke yake kimya kimya akiwa na imani kuwa
kishamaliza kesi aliyokuwa nayo na akawa na furaha tele akaendelea
kufanya mambo yake kama kawaida.
Je, mpenzi msomaji unadhani itakuaje siku ya Ijumaa
tatu Jenifer na baba yake wakienda wote shule ikiwa baba yake na Jenifer
anajua kuwa mwalimu anamtaka binti yake wakati sio kweli unadhani nini
kitatokea kati ya mwalimu na mzazi wake na Jenifer? Usikose muendelezo
wa hadithi hii sehemu ya tatu.
No comments:
Post a Comment